HabariMilele FmSwahili

Mudavadi kuwania kiti cha urais 2017

Kiongozi wa chama cha Amani National Congress ANC Musalia Mudavadi ametangaza nia yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017. Hii ni baada ya kutembelea eneo la aliyekuwa mfalme wa jamii ya Wanga Nabongo Mumia huko Mumias ili kupata baraka zake. Akiongea katika eneo hilo Mudavadi anasema tayari amekutana na viongozi wa Magharibi akiwemo Moses Wetangula, Bifwoli Wakoli, Francis Atwoli na Cyrus Jirongo na kukubaliana kumuunga mkono kiongozi mmoja kutoka eneo hilo.

Show More

Related Articles