HabariMilele FmSwahili

Wanachama wa TNA kutoka Nyanza kukihama chama iwapo seneta Joy Gwendo atafurushwa chamani

Baadhi ya wafuasi wa chama cha TNA kutoka nyanza wametishia kukigura chama hicho iwapo seneta mteule Joy Gwendo atafurushwa chamani humo.Wakiongozwa na Charles Amenya na Kevin Ondeyo wafuasi hao wamesema kuwa Gwendo ndiye tegea yao pekee chamani humo.Wamefutilia mbali madai kuwa Gwendo ni kibaraka wa ODM.Wamemtaka mwenyekiti wa chama cha TNA Joshon Sakaja kuingilia kati hali hiyo ili kuzuia udhibiti wa chama hicho eneo hilo.

Show More

Related Articles