HabariPilipili FM NewsSwahili

Huenda Masomo Yakatatizwa Na Mgogoro Wa Nyongeza Ya Mshahara Kwa Walimu.

Masomo katika shule za umma huenda yakatatizwa kuanzia jumatatu ya tarehe 31 mwezi huu, ikiwa ni mara ya pili mwaka huu, ambapo walimu wamesema huenda wakakosa kufika kazini kufuatia mgogoro unaoendelea baina yao na serikali wa malipo ya mishahara yao.

Shule zinatarajiwa kufunguliwa kwa muhula watatu ambao mwisho wake maelfu ya wanafunzi wanatarajiwa kufanya mitihani yao ya darasa la 8 na pia kidato cha nne.

Wazazi pamoja na viongozi wa shule, wamekuwa na matumaini ya kupatikana ufumbuzi wa mgogoro unaoendelea, ambapo tayari wazazi wengi wamenunua vifaa hitajika kwa ajili ya matayarisho ya wanafunzi kurudi shuleni kwa muhula wa tatu.

Mapema wiki iliyopita mahakama ya juu iliiambia serikali kuwalipa walimu nyongeza ya mishahara ya kati ya asilimia 50 na 60 kama ilivyo agiziwa na mahakama ya viwanda, ambapo sasa vyama vya walimu vinadai kuwa walimu hawatorudi kazini hadi serikali izingatie agizo la nyongeza ya mishahara.

Show More

Related Articles