HabariPilipili FM NewsSwahili

Waganga Tapeli Waonywa Kaunti Ya Kwale.

Naibu kamishna eneo la Kinango kaunti ya Kwale Moses Ivuto amewaonya waganga wanaoshirikiana na wananchi kwa madai ya kuwatambua washukiwa wa uchawi, akisema kuwa atakayepatika atakabiliwa kisheria.

Akizungumza kwenye mkutano na wakaazi eneo hilo, Ivuto amesema baadhi ya waganga wamechangia pakubwa ongezeko la visa vya mauaji, jambo ambalo amesema wao kama viongozi hawatalivumilia.

Aidha ameeleza kuwa waganga hao wanadaiwa kuwadanganya wenyeji kuwa wanauwezo wakuwatambua washukiwa wa uchawi wanao hangaisha wenyeji, jambo ambalo amelitaja kuwa la uongozi potovu na lenye kusababisha uhasama katika jamii.

Ivuto amedokeza kuwa tayari oparesheni ya kuwasaka waganga wanaodaiwa kuhusika na visa hivyo umeanzishwa katika maeneo tofauti kaunti ya kwale.

Show More

Related Articles