HabariPilipili FM NewsSwahili

Nkaiseri Atoa Hakikisho La Kudhibiti Uhalifu Nchini.

Waziri wa usalama wa nchi Joseph Nkaisery amesema serikali kupitia vyombo vya usalama imeweza kudhibiti hali ya usalama humu nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mombasa baada ya kikao maalum na viongozi wa usalama kanda ya pwani, Nkaisery amesema serikali imetambua changizo la ukosefu wa usalama katika maeneo mbali mbali ya nchi, na kwamba tayari wameweka mikakati kuhakikisha wananchi na wageni wanaozuru taifa hili wako salama.

Nkaisery amesema tayari serikali imebuni mbinu mbadala ili kukabiliana na jinamizi la utumizi wa mihadarati ambao umetajwa kama moja ya changizo la ukosefu wa usalama.

Kauli  ya waziri wa usalama humu nchi inajiri siku chache tu baada ya rais uhuru Kenyatta kuagiza viongozi kanda ya pwani kushirikiana na vyombo vya usalama ili kukabiliana na ulanguzi wa mihadarati.

Show More

Related Articles