HabariPilipili FM NewsSwahili

Msako Kufanywa Katika Maduka Ya Dawa Kote Nchini.

Bodi ya dawa na sumu nchini sasa ina mikakati mipya ya kupambana na watu ambao  wanauza dawa kinyume cha sheria ,kwani  kuna takriban maduka asilimia 20 ya dawa ambayo hayazingatii kanuni hitajika kuhusiana na uuzaji wa dawa.

Mkaguzi wa dawa katika bodi hiyo kanda ya pwani daktari Azaria Tola amebaini kuwa sasa wanampango wakufanya ukaguzi masaa ya jioni na hata usiku, kwani maduka mengi ya dawa almaarufu ‘Chemists’ yanayoendesha biashara kinyume cha sheria hufunguliwa masaa hayo ya jioni.

Wakati huohuo wazazi wametakiwa kuwa makini wanapopeleka watoto wao kusomea masuala ya dawa ,ili kuepuka kuwapeleka kwenye taasisi ambazo hazijasajiliwa.

Show More

Related Articles