HabariPilipili FM NewsSwahili

Changamoto Yatolewa Kwa Wafanyibiashara Mjini Mombasa.

Changamoto imetolewa kwa jamii ya wafanyibiashara katika ukanda wa pwani hususan kaunti ya Mombasa kuwa na meli yao binafsi ya kusafirisha mizigo hatua hii ikilenga kuongeza mapato kwa serikali ya kaunti pamoja na kuimarisha ukuaji wa uchumi.

Akiongea katika warsha ya kuelimisha jamii ya wafanyibiashara kuhusu mamlaka ya soko la mtaji,mwenyekiti wa muungano wa wafanyibiashara nchini James Mureu amesema ni jambo la kusikitisha kuona kwamba mji wa Mombasa hauna meli yake binafsi licha ya kuwa na bandari.

Mureu amesema muungano huo kwa ushirikiano na mamlaka ya soko la mtaji wanapanga kuunda kituo cha kusuluhisha migogoro kati ya wafanyibiashara mapema mwaka ujao ili kuwaepushia hasara wanayokadiria kila mara wanapofika mahakamani.

Ameitaka serikali kutoa mazingara mazuri kwa wafanyibiashara kuendesha biashara zao pamoja na kujenga uhusiano mzuri kati ya sekta ya umma na sekta ya kibinafsi.

Show More

Related Articles