HabariMilele FmSwahili

Kampeni dhidi ya dawa za kulevya pwani kung’oa nanga jumanne

Rais Uhuru Kenyatta amewaumuru tena wabunge na wakuu wa usalama eneo la Pwani kuanzisha kampeni ya kupambana na ulanguzi na matumizi ya dawa za kulevya eneo hilo. Akihutubia ujumbe wa watu 800 waliojumuishwa wabunge katika ikulu ndogo ya Mombasa rais anasema ni sharti wazazi na wenyeji kushiriki kampeni hiyo ili kuwanusuru maelefu ya vijana walioathirika.akiunga mkono agizo hilo la rais waziri wa maswala ya ndani Jospeh Nkaissery amesema wizara yake itaongoza kampeni hiyo jinsi ilivyoendesha kampeni ya kuwakabili wagemaji na wanaobugia pombe isiyofaa.

Show More

Related Articles