HabariMilele FmSwahili

Zaidi ya nyumba 10 zateketea moto Molo

Zaidi ya familia 10 kutoka mtaa wa Mutirithia mjini Molo zimeachwa bila makao baada ya moto mkubwa kuteketeza nyumba zao. Moto huo ambao chanzo chake bado hakijabainika umeteketeza zaidi ya nyumba kumi zilizotengenezwa kwa mbao. Mmoja wa waathiriwa Boniface Kamau ameisuta serikali ya kaunti ya Nakuru kwa utepetevu kukabiliana na moto huo huku akitoa wito kwake na wasamaria wema kuwapa usaidizi.

Show More

Related Articles