HabariPilipili FM NewsSwahili

Faida Za Kuagiza Sukari Kutoka Mataifa Ya Nje.

Utafiti wa benki ya dunia unaonyesha kuwa ingekuwa bora Kenya kuagiza sukari ya bei nafuu kutoka nje kuliko kudumisha mifumo ya sasa ya uzalishaji bila ufanisi.

Utafiti huo umeonyesha kuwa iwapo Kenya itaagiza sukari kutoka nje, itainua maisha ya takriban familia elfu 40 kutoka kwa umasikini kwa sababu itapunguza matumizi yao.

Imebainika kuwa sukari ni bidhaa muhimu sana kwa wakenya na kwamba hawako tayari kuwacha kuitumia bidhaa hiyo hata baada ya bei yake kuongezeka, jambo ambalo wataalam wamesema husababisha hata watu masikini kuachana na bidhaa nyinginezo, huku mtu mzima akidaiwa kutumia takriban shilingi elfu 2 mia moja na hamsini kwa bidhaa hiyo kwa mwaka.

Utafiti huo pia umeonyesha kuwa familia masikini katika maeneo ya mashambani na pia mjini ndio wanunuzi wakuu wa kiwango kikubwa cha sukari na kwamba wao ndio watafaidi zaidi na bei ya chini ya bidhaa hiyo.

Takriban zaidi ya familia elfu 4o huenda zikaepukana na umasikini iwapo bei ya sukari itapunguzwa kwa asilimia 20 kiwango ambachpo kinakadiriwa kupunguza umasikini kwa asilimia 1.5 kote nchini.

 

Show More

Related Articles