HabariMilele FmSwahili

Swala la uhuru wa kupokea habari nchini kuangaziwa leo

Shirika la transparency international linakutana asubuhi ya leo na tume ya wanasheria kutoka kanda ya afrika mashariki kuzungumzia swala la uhuru wa kupokea habari humu nchini.Katika mkutano huo mswada kuhusu uhuru wa kupata habari mwaka 2015 unatarajiwa kuangaziwa pakubwa.Shirika hilo linanuia kuhakikisha uhamasisho kuhusu umuhimu wa kupitishwa kwa mswada huo ili kuwapa wakenya uhuru wa pokea habari.Mswada huo uliwasilishwa bungeni na mbunge Priscilla Nyokabi.

Show More

Related Articles