HabariPeople DailyPilipili FM NewsSwahili

Wazazi Watakiwa Kushirikiana Na Serikali Kukabiliana Na Tatizo La Ugaidi.

Serikali imewataka wazazi wa vijana wanaodaiwa kwenda nchini somalia na kujiunga na kundi la al shabbab kushirikiana na maafisa wa polisi ili kuwasaidia kuwarudisha humu nchini.

Rais Kenyatta amesisitiza kuwa ugaidi hauna uhusiano na dini yoyote humu nchini huku akiwataka viongozi wa kidini na wale wa kisiasa kushirikiana na polisi katika kuwashinikiza vijana dhidi ya kujihusisha na shughuli za kigaidi.

Rais Kenyatta amewataka maafisa wa polisi kuwapokea vyema vijana hao pindi wanaporudi humu nchini na kuwasaidia kwa kuwapelekeka kwenye vituo vya kurekebisha tabia.

Matamshi ya rais Kenyatta yanajiri siku chache tu baada ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kutoa ripoti kuwa zaidi ya vijana 30 wa ukanda wa pwani wanaodaiwa kujihusisha na shughuli za kigaidi hawajulikani waliko.

Show More

Related Articles

Check Also

Close