HabariPilipili FM NewsSwahili

Rais Kenyatta Aagiza Oparesheni Kuanzishwa Dhidi ya Walanguzi Wa Mihadarati.

Rais uhuru Kenyatta ameamrisha asasi za kiusalama katika ukanda wa Pwani hususan kaunti ya Mombasa kuanzisha oparesheni dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya ikiwemo pombe haramu huku akiwataka wanasiasa kuwa katika mstari wa mbele katika kampeni dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya humu nchini.

Rais Kenyatta amesisitiza kuwa serikali haitolegeza kamba dhidi ya walanguzi kando na kuharibu vifaa vyoyyote vitakavyopatikana kutumiwa katika kuendeleza biashara hiyo .

Akizungumza mjini Mombasa uhuru amezitaja dawa za kulevya kuwa chanzo kikuu cha hali duni ya usalama humu nchini ,huku akizitaka asasi za kiusalama hususan halmashauri ya bandari ya Mombasa kuwa waangalifu .

Rais Kenyatta ameawataka vijana kujihusisha na miradi ya maendeleo kama vile sekta ya kilimo ili kukabiliana na suala la uhaba wa chakula humu nchini.

Show More

Related Articles