HabariPilipili FM NewsSwahili

Wabunge Wanawake Kutafuta Msaada Kupitisha Muswada Wa Usawa wa kijinsia.

Wabunge wanawake wameonyesha matumaini kwamba mapambano ya kutekeleza usawa wa kijinsia katika uteuzi wa nyadhfa za umma na siasa uko karibu kutimia.

Katika kikao cha mahojiano mapema leo, Wabunge hao wanawake wameonyesha juhudi zao mpya zinazonuia kuwashawishi wabunge wenzao wanaume kujiunga na wabunge 68 wanawake bungeni kupata idadi ya wabunge 233 ili kuupitisha mswada huo.

Mbunge wa Runyenjes Cecily Mbarire amesema hatua hiyo inawezekana ambapo tayari wameanza mchakato wa kuwashawishi wabunge wenzao wa kiume.

Kupitia mikutano yao ya kutangaza mswada huo kwa wabunge wanaume ili kuungwa mkono, Mbarire amesema wabunge 61 tayari wameahidi kuunga mkono wanawake kushinikiza utekelezaji wa mswada huo.

Mbunge huyo pia amewataka wanawake wengine nje ya bunge kutumia uhusiano wao na wabunge wanaume bungeni kuwaomba kuupitisha mswada huo.

Show More

Related Articles