HabariPilipili FM NewsSwahili

lawama Zakumba Kiwanda Cha Sukari Kaunti ya Kwale.

Usimamizi wa kiwanda cha uzalishaji sukari kiscol huko Ramisi kaunti ya Kwale unalaumiwa kwa kukwepa kulipa ushuru kwa serikali ya kaunti hiyo huku ukidaiwa kutumia mbinu fiche kusafirisha sukari hiyo.
Kulingana na mwakilishi wa wadi ya Puma ambaye pia ni kiongozi wa walio wachache katika bunge la Kwale James Dawa ,hatua hiyo ni ya kurudisha nyuma maendeleo ikizingatiwa kuwa maendeleo hutokana na ushuru unaotozwa wawekezaji.
Dawa ametoa changamoto kwa utawala wa kaunti hiyo kuweka mipangilio mwafaka kuhusiana na uwekezaji ,ili kuona kuwa unafaidisha wakaazi na serikali ya kaunti kwa jumla kwani amedokeza kuwa usimamizi huo umekumbwa na kasumba za unyanyasaji.

Show More

Related Articles