HabariMilele FmSwahili

Mashirika ya kuwatafutia wakenya ajira uarabuni walalamikia serikali

Mashirika ya kuwatafutia wakenya ajira katika mataifa ya uarabuni yamelalamikia marufuku iliyowekwa na serikali na kusema imechangia mateso wanayopitia wakenya wanaoajiriwa katika mataifa hayo. Mashirika hayo yanadai marufuku hiyo imechangia wakenya wengi kupelekwa katika mataifa hayo na mashirika ambayo hayajaidhinishwa. Mwenyekiti wa muungano wa kuangazia maslahi ya wakenya walio nje ya nchi David Njoroge ameitaka serikali kuyakagua mashirika ya uajiri na kuweka sheria kali za kukabili walanguzi wa watu

Show More

Related Articles