HabariMilele FmSwahili

Marekani imekumbatia hatua ya Salva Kiir kutia sahihi mkataba wa amani

Ikulu ya rais ya Marekani imekumbatia hatua ya rais wa Sudan Kusini  Salva Kiir kutia sahihi  mkataba wa amani kumaliza mgogoro ambao umekuwa ukishuhudiwa nchini humo.Hata hivyo ikulu hiyo imeonya kuwa kutiwa sahihi kwa mkataba huo kusiandamane na masharti au mapendekezo yoyote kutoka pande mbili husika.Imemtaka Kiir kuzingatia mkataba huo na kuanza shughuli za kurejesha nchi hiyo katika hali yake ya kawaida.
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesaini mkataba wa amani hapo jana kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 20 lakini pia ametowa orodha ya mashaka yake na kuonya kwamba makubaliano hayo yumkini yasidumu.Kiir amesema kwamba makubaliano wanayosaini leo hii yana mambo mengi ambayo inabidi wayakatae.Amesema iwapo mambo hayo yenye mashaka yatapuuzwa jambo hilo halitakuwa na maslahi kwa haki na amani ya kudumu.

Show More

Related Articles