HabariSwahili

Mahakama Kuu Yampokonya Dhamana Feisal.

Mahakama kuu mjini mombasa imefutilia mbali dhamana ya shilingi milioni kumi iliyokua imepewa kwa Faisal Ali Mohamed mshtakiwa wa ulanguzi wa pembe 314 za ndovu zilizo kamatwa mnamo mwezi juni mwaka jana.

Akitoa uamuzi huo jaji wa mahakama kuu Martin Muya amesema mahakama ya chini haikua na uwezo kikatiba kubatilisha uamuzi uliotolewa na mahakama kuu hapo awali ambao uliagiza faisal kubaki kizuizini, Muya pia ameongeza kusema mawakili wa mshatakiwa huyo walikosea kurudi kwenye mahakama ya chini kuomba dhamana ila wangepaswa kufanya maombi yao kwa mahakama ya rufaa. Hii ni mara ya nne kwa mahakama kuendelea kudinda kumwachilia kwa dhamana mshtakiwa huyo ambaye anatajwa na upande wa mashtaka kuwa kuachiliwa kwake huenda akatoroka vikao vya kesi hio ambayo tayari imeshaanza kuskizwa. Uamuzi wa awali wakuachiliwa kwa dhamana ulitolewa na hakimu Davis Karani ,ambaye jaji Muya ameagiza ajieke kando na kesi hio.

Show More

Related Articles