HabariSwahili

Msichana Afariki Baada Ya Kubugia Sumu.

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 21 amefariki baada ya kunywa sumu nyumbani kwao katika kijiji cha Shakahola-Chakama wilayani Magarini kaunti ya Kilifi.
Shaban Ziro Luganje ambaye ni kakake msichana huyo amesema Kadzo Ziro mwenye ujauzito alikuwa mwanafunzi wa chuo cha kiufundi katika eneo hilo, baada ya kutoka chuoni jana jioni alijifungia chumbani mwake na kutekeleza kitendo hicho.

Show More

Related Articles