HabariMilele FmSwahili

Waititu anasakwa na polisi kwa madai ya kuwachochea wafanyibiashara

Mbunge wa kabete Ferdinand Ngugi Waititu anasakwa na polisi kutoka kikuyu kwa madai ya kuwachochea wafanyibiashara katika soko la Wangige. Hii ni baada ya kuwasilishwa kwa lalama kutoka kwa katibu wa kaunti hiyo Fred Kitema na waziri wa maji na mazingira Esther Njuguna kuwa Waititu aliwachochea wafanyibiashara hao waliotekeleza uharibiwa wa mali ya kaunti ya Kiambu. Wafanyibiashara hao walizua vurugu baada ya mkutano na Waititu kabla ya kupeleka taka kwenye afisi mmoja wa wasimamizi wa wadi Evans Kariuki.

Show More

Related Articles