HabariMilele FmSwahili

Wauguzi Kakamega wakaidi wito wa kushiriki mgomo

Wauguzi kaunti ya Kakamega wamekaidi wito wa kushiriki mgomo. Wakiongozwa na katibu wao Renson Buluma wauguzi hao wamemtaka katibu mkuu wa muungano huo nchini Seth Panyako, kushughulikia maswala ya wauguzi walio na matatizo katika kaunti tofauti nchini. Wameongeza kaunti hiyo imeweka mikakati ya kutosha ya kuajiri wauguzi, huku wengine wakipandishwa vyeo pamoja na kupokea nyongeza ya mishahara.

Show More

Related Articles