HabariSwahili

Wazee Wa Kaya Wadai Kukamatwa Kinyume Cha sheria Na Polisi.

Hali ya sintofahamu imeibuka kati ya viongozi wa kaya na naibu kamishna katika wilaya ya Kisauni Julius Kavita baada ya wazee hao kudai kwamba walikamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi kinyume cha sheria.

Kulingana na mzee Dadu Kituku Mbaruku wao walikuja kuleta utulivu walipoarifiwa kwamba vijana wanaleta fujo kuhusiana na swala la ardhi katika eneo bunge la Kisauni lakini kilichowashangaza ni kukamatwa kwao bila ya hatia yoyote.

Show More

Related Articles