BurudaniSwahili

Wasanii Wa Pwani Wanabweteka Na Umaarufu Finyu Afunguka Kidis.

“Wasanii wa pwani wamejisahau na walikotoka wanabweteka na umaarufu finyu ambao wameupata na hawana lolote ila kujifurisha nakumea majipu ya makwapa nakujitangaza kuwa miungu ya mziki pwani”.Hii ni kauli ya msanii Kidis The Jembe ambaye alifunguka wakati akihojiwa kwenye kipindi cha Zinduka na Kahawa Uthungu ndani ya kituo tajika ndani ya pwani Pilipili fm. Kidis aliendelea kufunguka na kusema wakati wakuimba dis songs ulipitwa na wakati na yeye binafsi haezi poteza wakati wake kuingia ndani ya studio kuimba nyimbo ya kukashifu mtu.

Wakati huohuo msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya Viroboto alisema hakushangazwa na kitendo cha baadhi ya wasanii ambao waligomea kumsabahi wakati wa sherehe za vijana zilizofanyika kwenye uwanja wa kaunti mjini Mombasa.

Kidis alimalizia kwa kusema soko la mziki pwani bado halijafikia kiasi cha mtu kujitanua na kujiona amefika.

Show More

Related Articles