HabariMaarufu zaidiMilele FmSwahili

Je Waiguru ni Mfisadi ?

Shinikizo la kumtaka waziri wa mipango na ugatuzi Ann Waigiru kuondoka afisini zimeendelea kutolewa kufuatia tuhma za ufisadi katika shirika la huduma kwa vijana NYS.Mbali na viongozi wa upinzani wanaotaka ukaguzi wa fedha kuendeshwa dhidi kuhusu sakata ya milioni 862 ya uagizaji, gazeti la people daily limebaini kuwa NYS hawajaridhishwa na jinsi Waiguru amekuwa akiendesha shughuli katika shirika hilo.Gazeti hilo limewanukuu baadhi ya wakuu wa NYS wanaomlaumu Waiguru kwa kutaka kuendesha shughuli za shirika hilo binafsi.Inadaiwa amekuwa akiwahangaisha wakuu hao kwa kuteka baadhi ya miradi iliyoanzishwa nao na kuifanya kuonekana imepangwa na wizara yake.Aidha suala la uteuzi wa wakuu wa NYS pia limechochea shinikizo la kutaka aondolewe kutoka nafasi hiyo.

Also read:   UhuRuto wajibu upinzani kuwa Jubilee imesheheni wafisadi
Show More

Related Articles

Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker